EPL kutumia teknolojia ya offside msimu ujao

LONDON, Ligi Kuu ya England maarufu Premier league itaanza kutumia teknolojia ya kung’amua kama mchezaji yupo kwenye eneo la kuotea ‘offside’ inayojulikana kama Semi-Automated offside technology.

Uamuzi huo umefikiwa mchana wa leo baada ya klabu zinazoshiriki ligi hiyo pendwa duniani kukubaliana na mpango huo ambao unatazamiwa kupunguza utata zaidi katika masuala hayo ya offside.

Taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya ligi hiyo leo Aprili 11, 2024 inaeleza kuwa vilabu vimekubaliana kwa kauli moja kuanzishwa kwa Teknolojia hiyo inayotazamiwa kuleta urahisi wa kugundua matukio hayo kwa waamuzi na kuongeza ladha mpya na kuondoa utata hasa kwa wafuatiliaji wa ligi hiyo kwa njia ya Televisheni.

Teknolojia ya Semi-Automated Offside Technology ilitumika kwa ufanisi mkubwa katika Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2022 lilofanyika nchini Qatar na inakuwa teknolojia ya tatu kubwa kuingizwa kwenye soka baada ya teknolojia ya mstari wa goli, (Goal line Technology) na teknolojia ya usaidizi wa waamuzi kwa video Video Assist referee (VAR)

Habari Zifananazo

Back to top button