‘Kuna udanganyifu vipimo vya kopo, ndoo’

DAR ES SALAAM; WAKALA wa vipimo (WMA) umewataka wananchi kuachana na kununua bidhaa katika makopo, visado na ndoo na badala yake kutumia mizani sahihi ya bidhaa, Ili kukwepa udanganyifu.

Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa WMA, Paurus Oluochi amesema hayo leo Dar es Salaam katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ‘Sabasaba’ yanayoendelea.

Amesema kwa kununua bidhaa katika vyombo hivyo inapunguza ujazo kwa kuwa wapo wauzaji wanaopunguza ujazo wa vyombo hivyo na kwamba ni muhimu wananchi kutumia mizani sahihi.

Soma pia:https://habarileo.co.tz/rumbesa-chanzo-kipato-kushuka/

Amesema pia Wakala huo unatoa wito kwa halmashauri nchini kuanzisha vituo vya mauzo, vikiwa ni mizani sahihi vitakavyosaidia wakulima kupeleka mazao yao na kupimwa na kukagua uzito wa gunia, ili usizidi kilo 100 na kuepuka lumbesa.

Amesema kwa mujibu sheria ya vipimo sura 340, inaelekeza namna mazao ya shamba yanatakiwa kufungashwa kwamba yasizidi uzito wa kilo 100 na kwamba wanaojaza tofauti na sheria hiyo ni ukiukwaji na hatua zinaweza kuchukuliwa.

 

Habari Zifananazo

Back to top button