Erling Haaland ‘avurugwa’ kukosa Kombe la Dunia

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Erling Haaland amehuzunishwa kuona baadhi ya wachezaji wenzake wakisafiri kwenda kushiriki michuano ya Kombe la Dunia hali yakuwa timu yake ya Norway haijafuzu mashindano hayo.

Akizungumza na shirika la habari la ‘Reuters’ Haaland amesema itakuwa ni ndoto yake siku moja kucheza mashindano hayo huku akitabiri kuwa timu ya Taifa ya England ina uwezekano mkubwa wa kushinda Kombe la Dunia.

Nyota huyo anayekipiga Ashton United kwa mkopo wa siku 28, ameeleza kuwa kama England itafanya hivyo inabidi ihakikishe inaifunga timu za Argentina, Brazil na Ufaransa ambao wanaonekana kuwa na vikosi bora mwaka huu.

Licha ya kukosa Kombe la Dunia la 2022, Haaland alisema hajakata tamaa kufikia mashindano hayo.

“Natumai nitachezea Norway na ndoto yetu na ukweli, jambo kubwa tunaloweza kufanya ni kufika kwenye Kombe la Dunia au Euro,”ameongeza Haaland.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x