Ewura yamwaga mamilioni Iringa

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imechangia Shilingi Milioni 20 mkoani Iringa zitakazotumika kusaidia kukamilisha uzio wa shule ya sekondari ya wasichana Iringa na maadhimisho ya maonesho ya utalii ya siku tano ya Karibu Kusini yaliyoanza leo mjini Iringa.
Mchango huo ulikabidhiwa leo Novemba 9,2022  kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego wakati akifungua Baraza la Wafanyakazi la Taifa la Uwura linalofanyika mjini Iringa kwa siku tatu.
Akikabidhi mchango huo Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Mhandisi Modestus Lumato amesema kwa kupitia baraza hilo watajadili taarifa za utendaji kazi za mwaka 2021/2022 na motisha za wafanyakazi ili kuongeza chachu ya utendaji.
Aidha, Dendegu ameshukuru  kwa mchango huo na kuahidi kuhutumia kwa malengo yaliyokusudiwa kwani  baraza la wafanyakazi ni jukwaa muhimu mahala pa kazi na ni nyenzo muhimu katika kuboresha mazingira mazuri ya kazi.
Pia Dendegu aliwataka wafanyakazi kufuatia  njia sahihi za kudai haki zao na kujiepusha na mbinu zinazochochea migogoro kazini.

Habari Zifananazo

Back to top button