FABREGAS astaafu soka, awa kocha

KIUNGO raia wa Hispania, Cesc Fabregas ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 36.

Fabregas alianza soka kwenye timu ya vijana akiwa FC Barcelona mwaka 1997 ambapo alijiunga na Arsenal mwaka 2003 akiwa na ‘The Gunners’ Fabi alicheza mechi 212 na kufunga mabao 35.

Fabregas alidumu na Arsenal mpaka mwaka 2011 ambapo alijiunga na Barcelona kwa mara nyingine.

2014 aliondoka Barcelona akiwa amecheza michezo 96 na kufunga mabao 28. Alijiunga na Chelsea mwaka huohuo.

Akiwa Chelsea alicheza michezo 138 na kufunga mabao 15. Mwaka 2019 alijiunga na Monaco ya Ufaransa, akiwa klabuni hapo alicheza michezo 54 na kufunga mabao 3 pekee.

Baada ya hapo 2022 alijiunga na timu ya daraja la chini ya COMO kutoka Italia, hii leo ametangaza kustaafu.

1x World Cup 🏆
2x Euros 🏆
2x Premier League 🏆🏆
1x UEFA Super Cup 🏆
1x Club’s World Cup 🏆
1x La Liga 🏆
1x Community Shield 🏆
2x FA Cup 🏆🏆
1x English League Cup 🏆
1x Copa del Rey 🏆
2x Spanish Super Cup 🏆🏆

Baada ya kutangaza kustaafu soka, ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Como FC ya nchini Italia.

“Huu ni wakati sahihi kuanza kazi yangu kama kocha mkuu.” amesema Fabregas.

Habari Zifananazo

Back to top button