Fahamu Guardiola anavyompa majukumu Bernado

JINA lake ni Bernaldo Mota Veiga de Carvalho e Silva, alizaliwa Agosti 10, 1994 huko nchini Ureno katika jiji la kihistoria la Lisbon.

Bernaldo Silva ni mtoto wa familia ya baba mkandarasi, Mota Veiga de Carvalho e Silva na mama yake ambaye ni mwalimu wa shule, Maria Joao Mota Veiga, maisha yake ya utotoni alikua akipenda sana mpira na klabu aliyokuwa akishabikia ni Benfica.

Alipofikisha miaka 9 wazazi wake wakaamua kumpeleka kwenye chuo cha mafunzo ya soka cha SL Benfica ambapo chuo hiko kilimkuza kisoka mpaka walipofanikiwa kujipatia ubingwa kwenye mashindano ya soka la vijana katika msimu wa 2012/2013 kupitia klabu ya vijana wadogo Sl Benfica

Ilipofika Agosti 2013 alijiunga na klabu ya Benfica B na mechi yake ya kwanza kucheza kwenye klabu hiyo ilikua ni mechi ya ligi ya daraja la pili huko ureno (segunda liga) mechi hiyo iliwakutanisha Benfica dhidi ya Trofense katika msimu wa 2013/2014 na msimu huohuo walibeba mataji matatu na Bernaldo Silva alifanikiwa kuingia kwenye kinyang`anyiro cha tuzo za mchezaji bora msimu huo.

Nyota yake ilianza kung’aa pale tu klabu ya Monaco ya Ligi Kuu Ufaransa kuuona uwezo wake na kumchukua kwa mkopo kutoka Benfica mwaka 2014, uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi kwa uweledi mkubwa na akili alizonazo dimbani ziliifanya klabu ya Monaco kumchukua mazima ilipofika mwaka 2015.

Aliitumikia klabu ya Monaco mpaka 2017 wakati ambao kocha Pep  Guardiola anajiunga kuinoa miamba ya Uingereza Manchester City Bernaldo akawa usajili wake wa kwanza, amefanikiwa kuchuakua mataji kama  Carabao 4, kutoka msimu wa 2017/18 hadi 2020/21, pia waliweza kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu England 5, jambo kubwa zaidi waliweza kufanikisha ndoto ya mashabiki wa City kwa kuchukua kombe la UEFA Champions League mwaka huu 2023 kwa mara ya kwanza tangu klabu hiyo ianzishwe.

Bernaldo Silva ametumika katika nafasi nyingi dimbani akiongozwa na kocha wake ambapo mara nyingi ametumika kama winga wa kulia, pia ametumika kama kiungo mshambuliaji, Pep Guardiola hakuishia kumtumkia hapo tu muda mwengine timu inapohitaji kiungo mkabaji wakati wa mchezo Bernaldo hurudishwa chini kukaba na hufanya vizuri sana.

Kocha huyo mwenye asili ya Kihispania hakuishia hapo tu amemtumia Bernaldo katika nafasi ya beki wa kushoto jambo ambalo limedhihirisha uwezo mkubwa na wakipekee alionaoo mwamba huyo wa Kireno.

Bernaldo Silva ameongeza mkataba wa kuitumikia klabu ya Manchester City mpaka 2026, ni wazi kuwa Bernaldo ndiyo mchezaji wa muhimu sana kwa Pep Guardiola kwani hata kwenye mahojiano na waandishi wa habari anaeleza kuwa Bernaldo si mchezaji mweye takwimu kubwa za magoli lakini ni msaada mkubwa kwa Timu

“Bernaldo hajawahi kuwa mfungaji bora wala mtoa pasi za mwisho bora lakini anatusaidia kucheza vizuri”

Imeandaliwa na Vuai Abdallah

Tembelea //epaper.tsn.go.tz kusoma zaidi

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button