Fahamu mapito ya Prince William

LONDON, UINGEREZA; Siku ya kuzaliwa ni siku ya kutafakari maisha ya mwanadamu, ambapo wengi tumezoea kusherehekea, na hakuna shaka mtoto wa mfalme nchini Uingereza,  Prince William of Wales , anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na kutimiza miaka 42.

Siku hii inamfanya mwanamfalme huyu wa Uingereza kutafakari mambo mengi ya maisha yake alipotoka na kuelekea kwa maslahi ya Uingereza.

“William kwa sasa ana mambo mengi ya kutafakari kama Mfalme Charles III alivvyokuwa”, alisema mtaalam wa kifalme Jennie Bond.

Advertisement

Licha ya kukabiliana na changamoto katika maisha yake, Prince William ana majukumu mengi ya kushughulikia ikiwemo majukumu ya kitaifa na kifamilia.

Hivi sasa Prince William yuko katika kipindi kigumu, ambapo mwanzoni mwa Januari aligundua mke wake Kate Middleton anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani, huku Baba yake mzazi Mfalme Charles III naye akiwa katika maradhi yanayotajwa saraatani isiyojulikana.

Licha ya changamoto hizi, William ameendelea kupambana na kutimiza wajibu wake wa kusimamia familia yake ikiwa ni pamoja na uangalizi wa watoto kama baba, kuangalia afya ya mkewe na baba yake.

Katika ndoa yake, Prince William na Mkewe Kate wamejaaliwa kupata watoto watatu Prince George, Princess Charlotte na Prince Louis.

“Naweza kusema miezi ya hivi karibuni maisha ya William yamevurugika kutokana na majukumu magumu ya kifamilia “amesema Jennie.

Familia ya William tangu awali ilikuwa ni familia iliyokuwa na amani , upendo na ushirikiano mkubwa kuanzia mke na watoto Dimbwi hili kubwa la mawazo limeanza kumyemelea William wa Wales kuanza kufikiria uhai wa familia, usimamizi wa shughuli za kifalme kadhalika na hatma yake ya kuwa Mfalme wa Uingereza.

Matatizo ya afya ya Baba yake yanamfanya William kuwa na mawazo mengi ya kusimamia kasri ya Uingereza,
si jukumu dogo ni jukumu kubwa ambalo linahitaji utulivu wa kupanga na kufikiri ili jukumu hilo liweze kutekelezwa kwa ufanisi.

Licha ya kuwa na mtihani wa kuuguza baba yake mzazi William ameendelea kuwa karibu na Mfalme Charles kusaidiana katika majukumu mazito ya kifalme huku akiendelea na majukumu ya kifamilia.

Prince William Arthur Philip Louis alizaliwa katika Hospitali ya Mtakatifu Mary mnamo mwaka 1982 ni mtoto wa kwanza na halali wa Mfalme Charles III na Princess Diana.

Wakati William akizaliwa wanandoa hawa wawili waliokuwa na mapenzi makubwa walipendekeza majina kadhaa kwa ajili ya mtoto wao mpendwa kutoka kwa baadhi ya jamaa zao ikiwa ni Philip, Duke of Edinburgh na jina lingine lililopendekezwa lilikuwa la mjomba wake Lord Louis Mountbatten.

Wakati pia jina lake la pili la Arthur lilikuwa na nafasi kubwa ya kupewa Prince William, lakini Charles na Diana waliamua kuchagua jina lingine ili liweze kutumika kwa mtoto wao.

Heshima ya majina mengi ya kifamilia haikuwafanya wanandoa hawa kutoa majina hayo, lakini waliamini kuwa lipo jina ambalo litakuwa na nuru kwa mtoto wao .

Wakati wa kutafakari kwa kina wakagundua kuna jina moja la Mfalme mpya William ndilo linamfaa mtoto wao na hapo ndipo Jina la Prince William likapitishwa na kuidhinishwa na leo hii kutambulika kama “William of Wales “