Familia: Bruce Willis ana tatizo la akili

MUIGIZAJI Bruce Willis ana tatizo la akili la frontotemporal, familia yake imetangaza.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 67 aligunduliwa na aphasia – ambayo husababisha ugumu wa kuzungumza – katika msimu wa joto mwaka jana, lakini imeendelea na amepewa utambuzi maalum zaidi, familia ilisema.

Walionesha “shukrani zao za dhati kwa upendo”.

Familia iliendelea kusema tatizo la akili la frontotemporal ni la kawaida kwa watu walio na zaidi ya miaka 60.

“Hakuna matibabu ya ugonjwa huo, ukweli ambao tunatumai unaweza kubadilika katika miaka ijayo,” ilisema taarifa hiyo.

Willis alikuja kuwa maarufu katika miaka ya 1980 na 90 baada ya kuigiza katika filamu maarufu kama vile Die Hard, The Sixth Sense, Armageddon na Pulp Fiction.

Habari Zifananazo

Back to top button