DAR ES SALAAM; MBUNGE wa Jimbo la Monduli, ambaye ni mtoto wa Edward Lowassa, Fredrick Lowassa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupigania afya ya baba yao kabla ya kufikwa na umauti.
“Niseme ukweli kama isingekuwa mama Samia Suluhu Hassan, baba yetu asingefika hata hiyo juzi, mama Samia amekuwa ni ndugu, mama mzazi, mlezi wetu kwa kweli hatuna cha kumlipa, ” amesema Lowassa.
Amesema siku ambayo Rais Samia alikwenda Italia kwenye ziara ya kikazi, hali ya baba yake ilibadilika, hivyo alimtuma mkuu wa majeshi kusimamia matibabu ya baba yake.
“Watoto na wazazi wanaoshiriki shule za kata leo wanaomboleza, watoto na wazazi wanaokunywa maji Ziwa Victoria leo wanaomboleza, watoto na wazazi ambao wanasomesha watoto wao Udom leo wanaomboleza,”amesema Fredrick Lowassa.