Faraji atuma salamu kwa mpinzani wake

DAR ES SALAAM: Bondia Saidi Faraji ‘Kichwa Kisicho na Ubongo’ kutoka Mabibo ametoa kauli za kibabe kwa mpinzani wake, Lucas Onesmo wa Manzense Dar es salaam, kuelekea pambano lililopewa jina la ‘Hatukimbii Hatuogopi’ litakalofanyika Aprili 11, 2024 mkoani Morogoro.

Akizungumza jijini Dar es Salaam,wakati akiendelea na hamasa ya maandalizi ya pambano Faraji amesema yeye sio daraja la mafanikio kwa mabondia wanaochipukia.

“Nimejipanga vizuri kuhakikisha nawapa furaha mashabiki zangu kwa ushindi wa KO mbaya kwenye pambano langu atajuta kucheza na mimi.”amesema Saidi Torres.

Kwa upande wake mkufunzi wa bondia huyo Emmanuel Jabulan amesema ujio mpya wa Torres ni hatari hivyo mpinzani wake ajiandae kupokea kichapo cha aina yake siku hiyo.

 

Habari Zifananazo

Back to top button