Farasi watumika doria Ranchi ya Kongwa

DODOMA; FARASI walioko katika Ranchi ya Kongwa iliyoko jijini Dodoma, wamekuwa wakifanya doria katika eneo lenye ukubwa wa hekta 19,570.

Eneo la ranchi hiyo lina ukubwa wa hekta 38,000, kati ya hizo hekta 19,570 zinasimamiwa na ranchi hiyo na zilizobaki zimegawanywa katika vitalu vidogo na kupewa wananchi.

Meneja wa ranchi hiyo ya Kongwa Dodoma, Elisa Binamungu amesema wanatumia wanyama hao kufanya doria kwa sababu wana uwezo wa kuzungukia makundi matano ya mifugo.

” Ukiwa na farasi inapunguza wingi wa wachungaji, mchungaji mmoja mwenye farasi anaweza akazungukia makundi hata matano.

” Lakini kwa kuwa tuna maeneo mengi, mengine hayapitiki lakini farasi anaweza kupita eneo ambalo hata gari haliwezi kupita, pikipiki haiwezi kupita lakini pia na mwendo wa farasi ni rahisi hata kama kumetokea uvamizi katika maeneo yetu kuweza kuzuia.

“Kwa mfano kama wizi wa kuirudisha mifugo katika mikono yetu,”amesema na kusisitiza kuwa kazi kubwa ya farasi ni kufanya doria sio kwa ajili ya nyama.

Habari Zifananazo

Back to top button