Fati kukiwasha Brighton

MSHAMBULIAJI wa FC Barcelona, Ansu Fati anakaribia kujiunga na Brighton & Hove Albion kwa mkopo wa msimu mmoja.

Imeelezwa kutoka kwa mwandishi wa habari za michezo, Fabrizio Romano kuwa katika mkopo huo hakuna kipengele cha manunuzi ya jumla, hivyo mara baada ya msimu huu kuisha atarejea Camp Nou.

Fati mzaliwa wa Guinea Bissau atakamilisha usajili huo saa 24 zijazo, kwa mujibu wa mwandishi huyo.

Habari Zifananazo

Back to top button