FCC kukutanisha wadau wa mazingira na utalii
OGEZEKO la hewa ukaa linachangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabianchi yanaloleta athari katika ikolojia ikiwemo kudhibiti barafu ya Mlima Kilimanjaro kutoyeyuka na kuongeza idadi ya watalii nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) William Erio amesema tume hiyo imeandaa kongamano la wadau wa mazingira na utalii litakalofanyika Jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya madhimisho ya siku ya ushindani Duniani itakayofanyika Desemba ,5 mwaka huu.
Amesema mabadiliko ya mazingira yanaweza kuleta ukame hivyo lazima theluji iliyopo Mlima Kilimanjaro iendelee kuwepo kwa kuhakikisha mazingira yanatunzwa.
“Lazima tulinde mazingira na wale wanaofanya wanaofanya shughuli za utalii walinde mazingira ili kulinda theluji ya mlima Kilimanjaro kwani ndio inayoleta watalii wengi nchini na utalii kanda ya kaskazini umeshamiri sana”
Amesema kauli mbiu ya kongamano hilo ni “sera ya ushindani na mabadiliko ya tabia Nchi ambayo ni ya kidunia katika maadhimisho ya FCC na kwa upande wa Tanzania kauli mbiu ni ushindani na utalii endelevu”
Watu 120 watahudhuria kongamano hilo kwalengo la kutunza mazingira na mabadiliko ya tabia nchi kwani athari za kiikolojia zinaweza kudhibitiwa ili kuhakikisha kila mtu ananufaika na mazingira rafiki kwa binadamu na wanyama.