FCC kutumia Sh bilioni moja kuvutia wawekezaji

DAR ES SALAAM: KIASI cha Sh bilioni 1.56 kitatumika katika kuweka miundombinu ya kisasa ya TEHAMA kwa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) ili kukuza teknolojia na kurahisisha kazi za uwekezaji nchini.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya FCC kuingia mkataba wa ushirikiano na TradeMark Africa leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa FCC, William Erio (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa TradeMark Afrika, Elibariki Shammy (kulia) katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano Mei 27, 2024 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio amesema watakuwa na maboresho makubwa ya miundobinu ya ndani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) lakini pia watafanya mafunzo kwa wafanyakazi ili waweze kutumia mifumo itakayowekwa na mchakato utakuwepo kwa ufanisi.

“Tulizungumza na wenzetu wa TradeMark Afrika kama washirika wetu wa biashara na tulikubaliana  kuwa wakati umefika wa kuhakikishughuli zetu za kiutenda zinafanyika kupitia mfumo na kitakachofanyika katika mkataba huu serikali sasa inazungumzia digital na sasa dunia inaenda huko utahakikisha  utendaji wetu uende kwa utaratibu na kukidhi matarajio na mategemeo ya wale tunaofanya kazi zetu ambao wengi ni nje ya Tanzania,” amesisitiza.

SOMA: Biashara ya bidhaa bandia yaongezeka

Erio amesema zoezi  hilo linatarajiwa kutumia muda wa miaka mitatu ambapo kila kitu kitakamilika ndani ya miaka miwili na mwaka mmoja ni kuangalia matokeo na kujiridhisha kwamba kila kitu kinafanya kazi kama ilivyokusudiwa.

Amebainisha kuwa  faida yake ni wawekezaji kuwekeza kwa uharaka na mapema na watapata faida kwa wakati  huku nchi ikinufaika na matokeo ya uwekezaji huo kwa  kuongeza mapato,ajira na fedha za kigeni .

“Wawekezaji watakuja kufungua biashara na makampuni na wanaoenda FCC wakihitaji washirika wa kufanya nao biashara tunahakikisha hili kundi linapokuja tunafanya shughuli za kwa ufanisi kwani serikali imejikita kuvutia wawekezaji wanaleta fedha za kigeni ,kukuza teknolojia na kuongeza ajira wanaleta faida nchini.

Amesema muda wa kushughulikia maombi utakuwa mfupi zaidi na gharama za uwekezaji zitapungua.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa TradeMark Africa, Elibariki Shammy amesema wameweka fedha ya mbegu huku  mkakati wao  utaenda 2030 ambapo huo ni mkataba wa awali utakao saidia katika kupunguza gharama za kufanya biashara na kupunguza muda wa wawekazaji kupata mahitaji yao.

‘Itatunza afya za walaji tutawekeza pamoja na wao mwisho wa siku tukuze biashara  na kuna wadau tuko nao kwenye mazungumzo na tutarejea zaidi baada ya mpango huu kufanikiwa,” ameeleza Shammy.

Amesema wanaondoa vikwazo vinavyozuia biashara kufanyika ndani na nje ya nchi, kukuza  biashara ya kikanda na kimataifa.

Habari Zifananazo

Back to top button