FCT kuimarisha ushindani nchini

DAR ES SALAAM: Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, ametembelea Baraza la Ushindani (FCT) katika ofisi baraza zilizopo Dar es Salaam, ambapo alipokea taarifa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya chombo hicho na kutoa maelekezo ya kuimarisha utendaji kazi.

Katika ziara hiyo, Waziri Kapinga alipatiwa maelezo ya kina kuhusu FCT inavyosimamia mashauri ya ushindani, kulinda maslahi ya watumiaji wa bidhaa na huduma, pamoja na juhudi za kuhakikisha mazingira ya kibiashara nchini yanabaki kuwa huru, ya haki na shindani.

Aidha, alilipongeza baraza kwa hatua kubwa lilizopiga katika kukuza na kulinda ushindani wa haki sokoni.

Kapinga ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu na baraza hilo ili kuhakikisha majukumu yake yanatekelezwa kwa ufanisi zaidi, sambamba na dhamira ya Serikali inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha misingi ya uchumi na kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Msajili wa Baraza la Ushindani, Mbegu Kasikasi, amesema maelekezo yote yaliyotolewa na waziri yatatekelezwa kwa haraka ili kuongeza ufanisi wa kazi.

Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano, Baraza limepokea mashauri 156 na kati ya hayo, 152 yamesikilizwa na kutolewa maamuzi, ikiwa ni asilimia 96 ya mashauri yote, jambo linaloonyesha hatua kubwa katika utekelezaji wa majukumu yake.

Ziara hiyo imetoa dira mpya kuhusu nafasi ya FCT katika kukuza ushindani wa haki, kuongeza uwazi, na kuimarisha mazingira bora ya biashara nchini.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button