Fei Toto aitwa TFF zogo lake na Yanga

KIUNGO wa Yanga ya Dar es Salaam, ambaye ametangaza kuvunja mkataba na klabu hiyo, Feisal Salum ameitwa kwenye kikao cha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF.

Kwa mujibu wa barua inayosambaa mitandaoni, ambayo HABARILEO imeiona, iliyosainiwa na Herman Kidifu kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), inaonesha iliandikwa Desemba 31, 2022 na kikao kitafanyika kesho Jnauari 4, 2023 ofisi za TFF.

Hatua ya TFF kuitisha kikao cha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inatokana na malalamiko ya Yanga kuhusu mchezaji huyo kwa suala la mkataba wake.

Habari Zifananazo

Back to top button