Fei Toto atua Dubai
KINGO mahiri wa Tanzania aliyetangaza kununua mkataba wake na Yanga ya Dar es Salaam, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ yupo Dubai, Falme za Kiarabu akiwa katika mapumziko na katika sherehe za kuukaribisha Mwaka mpya.
Mwanandinga huyo ametua Dubai leo asubuhi akitokea Visiwani Zanzibar na kupokelewa na wenyeji wake.
” Tumempokea Fei Toto, tutakuwa naye hapa Dubai amekuja kupumzika,” amesema mmoj kati ya wadau wakubwa waliofika kumpokea, ambaye hakupenda jina lake litajwe.
” Sina nilichosahau, kwa sasa nipo hapa Dubai kupumzika baada ya hapo nitaamua timu gani niende kucheza mpira,” alisema kiungo huyo.
Feisal ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ alitangaza kununua mkataba wake na Yanga, lakini uongozi wa Yanga umekataa suala hilo na kusisitiza kuwa kiungo huyo bado mchezaji halali wa Yanga na mkataba wake utamalizika Mei mwaka 2024.