Fei Toto kuiomba Fifa atafute timu

KIUNGO mahiri nchini Feisal Salum ‘Fei Toto’, ambaye ana mgogoro na klabu yake ya Yanga ya Dar es Salaam, anakusudia kuliomba Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa), limruhusu apate timu dirisha hili la usajili, wakati mgogoro wake na Yanga ukiendelea.

Wakili Salum Nduruma anayemuwakilisha mchezaji huyo amesema leo kuwa wanakusudia kuiandikia barua Fifa, ikibidi mchezaji huyo atafute timu ya kucheza kwenye dirisha hili la usajili linaloendelea, huku taratibu nyingine za rufani zikiendelea.

“Hukumu tuliyopewa haina tofauti na taarifa iliyotolewa na TFF (Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania). Tunataka kuwaandikia FIFA kuwaelezea mazingira yote yalivyokuwa, ili kama inawezekana wakati Fei Toto anaendelea na rufaa aweze kusajiliwa hata kwa dirisha moja,” amesema Nduruma.

Akizungumza na UFM Redio leo Januari 11, 2023 Nduruma amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya kukiri kupokea nakala ya hukumu kutoka Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF.

Nduruma amesema kuwa mchezaji huyo ataendelea kupinga maamuzi hayo kwa sababu hayakumtendea haki.

Habari Zifananazo

Back to top button