KIUNGO wa Azam FC, Feisal Salum ametolea ufafanuzi fedha alizochangisha kutoka wa wadau mbalimbali kwa ajili ya kwenda CAS kutafuta haki yake dhidi ya waajiri wake wa zamani Yanga.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu yake mpya ya Azam, Feisal amesema hawezi kumrudisha fedha kila aliyemchangia hivyo ni bora kupeleka msikitini, kanisani na kuwapa yatima.
“Ile pesa iliyochangishwa siwafahamu waliotoa nitaipeleka kwa watoto yatima kwa sababu sjui ni nani aliyechangisha kwahiyo nimeona ni bora kuipeleka kwa wenye uhitaji.” amesema Feisal Salum.
Feisal na Yanga wamemaliza sakata lao baada ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu kuielekeza Yanga kufanya hivyo kisha itoe mrejesho baada ya kumaliza suala hilo.