KIUNGO mpya wa Azam Fc Feisal Salum ‘Feitoto, amesema anafuraha kubwa sakata lake na waajiri wake wa zamani kumalizwa na amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulimaliza sakata hilo
“Namshukuru Rais kwa kulimaliza hili jambo, nitazidi kumuombe katika majukumu yake”
“Nawashukuru pia mashabiki wa Yanga na Viongozi kwa upendo walionionesha”
Feitoto pia ametolea ufafanuzi juu ya fedha alizochangisha kutoka kwa watanzania akitaka kwenda CAS
“Ile pesa iliyochangishwa siwafahamu waliotoa nitaipeleka kwa watoto yatima kwa sababu sjui ni nani aliyechangisha kwahiyo nimeona ni bora kuipeleka kwa wenye uhitaji” amesema Feitoto
Kwa Upande wake Ofisa mtendaji mkuu wa Azam Fc Abdulkarim Amin ‘ Popat, amesema ni jambo jema sakata hilo limefika mwisho
” ” Namshukuru Rais kwa kulimaliza suala hili, nawashukuru pia Yanga kwa kulimaliza hili , mpira ni umoja na ni undugu tunawatakia kila la kheri Yanga kwenye mashindano wanayoshiriki” amesema Popat.
Feisal Salum amesaini kandarasi ya miaka mitatu Azam Fc hivyo atakuwa chamazi hadi mwaka 2026.