Feisal asimulia alivyosalitiwa na mpenzi wake
KIUNGO wa Azam FC, Feisal Salum ameeleza kuwa alikimbiwa na mpenzi wake aliyetaka kumuoa wakati wa sakata lake na klabu ya Yanga.
–
Feisal amezungumza hayo alipofanya mahojiano na MCL na kuongeza kuwa sakata hilo lilimuathiri kwenye masuala mengi ya kikazi na kijamii.
–
“Aliona kama maisha yangu ya soka tena basi ndio yameishia pale alishindwa kuvumilia na kuamua kutafuta mtu mwingine kitu kilichoniumiza zaidi ni hatua mbaya zaidi kwangu ikawa kwenda kuolewa tena nikiwa katikati ya lile sakata,”
–
“Sikuwa nimemuoa ila tulikuwa na mipango mingi ya maisha kati yetu, hakutaka kuvumilia kabisa nililazimika kuyapokea maamuzi yake hakukuwa na namna na sasa nimerudi uwanjani maisha mengine yataendelea tu.”Ameeleza Feisal.