Feitoto afunguka mazito sakata na Yanga

KIUNGO Feisal Salum ‘Feitoto’ leo amevunja ukimya na kueleza sababu ya mgogoro wake na Klabu ya Yanga.

Katika mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini Feitoto amesema mambo mengi waliyokubaliana kabla ya kusaini mkataba yalikuwa tofauti na yale aliyosaini kwenye mkataba hivyo na yeye alisaini mkataba huo bila kujua kama una dosari hizo.

“Mkataba umeandikwa kwa lugha ya kingereza na mimi siimudu lugha hiyo, makubaliano yalikuwa nisaini mkataba wa miaka miwili lakini nilisaini miaka mitatu bila kujua”Amesema Feitoto

Feitoto amesema hayupo tayari kurejea Yanga licha ya yeye na familia yake kuwa na mahaba mazito na timu hiyo.

” Mara zaidi ya mbili nimeambiwa kuwa nimeuza mechi inaniuma sana nakumbuka mechi ya Prisons na Kagera Sugar, napewa vitisho kuwa utarudi kwenu Pembab “Mimi sio mpemba mimi ni Mtanzania”

“Nilimpigia Ghalib simu ili kumueleza matatizo yangu lakini hakuwa akipokea simu yangu, baada ya hili sakata kuanza ndio akanipigia na mimi sikupokea maana zile ni dharau, mimi ni maskini ila haimanishi ndio unidharau” Feitoto.

Habari Zifananazo

Back to top button