KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum ‘Feitoto’ amesema hana tatizo lolote na klabu ya Yanga ila ana tatizo na Rais wa klabu hiyo, Mhandisi Hersi Said.
Kwenye mahojiano na chombo kimoja cha habari Feitoto amesema kuna tofauti kubwa mno kati ya kiongozi wa juu wa Yanga aliyepita na huyu aliyepo hivi sasa.
“Akiondoka Rais wa Yanga ninafunga vitu vyangu haraka na kurudi kwenye kambi ya Yanga”
Feitoto amesisitiza kuwa hatorudi nyuma kwenye kile anachokiamini.