Feleshi: Atakaekwamisha jitihada za serikali kukiona

MWANASHERIA Mkuu wa serikali, Dk Eliezer Feleshi amewataka majaji na mahakimu kuwaripoti wakili au mtendaji yoyote ambaye atakwamisha juhudi za serikali na mahakama katika kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi.

Feleshi ameyasema hayo leo, Februari Mosi, 2023 katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Chinangali mjini Dodoma.

Amesema, dhamira ya serikali ni kuona migogoro inayojitokeza katika maeneo mbali mba nchi inatatuliwa kwa njia zitakazowawezesha wadu kumaliza tofauti zao mapema ili wakajikite katika shughuli za uzalishaji

Advertisement

“Migogoro si tu  inatumia gharama kubwa katika utatuzi bali inasababisha mitaji ya uwekezaji kukaa bila uzalishaji uliotarajiwa na hivyo kukwamisha maendeleo yaliyokusudiwa pamoja na kuendeleza uadui.

Aidha, amesema kauli mbiu ya maadhishio ya siku ya sheria nchini kwa mwaka huu iwe msingi wa kuanza mwaka 2023 wa kazi za mahakama  kwa kuzingatia umuhimu wa kutatua migogoro iliyopo na itakayojitokeza kwa njia ya usuluhishi

Kauli mbiu ya mwaka  huu ni umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu, wajibu wa mahakama na wadau

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *