Fiesta yazinduliwa kwa staili yake

Fiesta yazinduliwa kwa staili yake

MSIMU wa Fiesta 2022 umezinduliwa juzi kwa staili ya aina yake kwa wasanii wa muziki kuonesha umahiri wao juu ya kontena la futi 40.

Hafla hiyo ya kuwatambulisha wasanii watakaolishambulia jukwaa kwenye msimu huu ilifanyika kwenye yadi ya makontena iliyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam ikihudhuriwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya waliokonga nyoyo za mashabiki katika tukio hilo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya msimu wa Fiesta 2022, Sebastian Maganga wamezindua mwaka mpya na tukio kubwa la burudani linalotimiza miaka 18.

Advertisement

Aidha, Maganga alisema msimu wa Fiesta unatarajia kuanza Septemba 17 kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa na baadaye kuhamia mikoa ya Tabora, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mtwara na Dar es Salaam.

Alisema kaulimbiu ya Fiesta 2022 ni ‘Weka Maneno’.

Baadhi ya wasanii waliotambulishwa juzi ni Abdul Kiba, Ally Kiba, Jux, Rayvanny, Marioo, Sarafina, Kundi la Weusi, Kussa, Mr Bluu, Coutry Boy, Maarifa, Stamina, Kayumba, Nay wa Mitego, Jay Melody, Young Lunya na Dogo Janja.

 

 

 

 

/* */