FIFA yaonya siasa Kombe la Dunia

SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu ‘FIFA’ limezionya timu zote zitakazoshiriki Kombe la Dunia nchini Qatar juu ya viashiria vyovyote katika kila vita vya kiitikadi au kisiasa vinavyoendelea katika baadhi ya mataifa.

Rais wa FIFA, Gianni Infantino na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Fatma Samoura wametuma barua kwa timu hizo wakipiga vita masuala hayo.  Baadhi ya ligi kama EPL na Laliga zilizonekana zikilitetea Taifa la Ukraine.

Katika barua hiyo imeeleza kuwa imekuwa ni maendeleo ya Kombe la Dunia iliyogubikwa na wasiwasi kuhusu mateso ya wafanyakazi wahamiaji wanaolipwa mshahara mdogo, kujenga miundombinu katika Taifa dogo la Ghuba na sheria za kibaguzi zinazoharamisha mahusiano ya watu wa jinsia moja.

“Tafadhali, sasa tuzingatie soka!

” Infantino na Samoura waliyaandikia mataifa 32 ya soka yatakayoshiriki Kombe la Dunia.

Habari Zifananazo

Back to top button