FIFA yashusha rungu Yanga

DAR ES SALAAM: KLABU ya Yanga imefungiwa kufanya usajili kwa kukiuka kanuni za Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA)

FIFA wamefikia uamuzi huo baada ya Yanga kukiuka Annexe 3ya kanuni ya uhamisho wa wachezaji (RSTP) ya shirikisho hilo.

Taarifa ya TFF imesema pamoja na masuala mengine, Yanga haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa mchezaji husika katika mfumo wa usajili (TMS) licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.

Kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) limeifungia Yanga kufanya usajili wa wachezaji wa ndani.

Habari Zifananazo

Back to top button