Filamu ya Eonii gumzo

FILAMU ya Eonii iliyoongozwa na Mtanzania Eddie Mzale, imeendelea kuwa gumzo kwenye maeeno mbalimbali na kumwagiwa sifa.

Filamu hiyo ambayo imeshinda Tuzo ya Filamu Bora ya Tamasha la  26 la ZIFF lilofanyika Zanzibar, imeibua wadau mbalimbali wa filamu hapa nchini.

Mkurugenzi wa tamsha la ZIFF Prof. Martin Mhando, amesema  ujio wa filamu hiyo una maana kubwa kwenye tasnia ya filamu nchini na hivyo kuamsha zaidi wasanii kufanya kazi kwa ubora mkubwa.

“Hii ni alama kubwa ya kukua kwa tasnia ya filamu nchini , filamu hii imetuheshimisha kama  filamu ya Binti ya Vuta N’kuvute ilivyofanya vizuri,” amesema Prof Mhando.

Ushindi wa Filamu hiyo katika Tamasha la ZIFF unakuwa ni ushindi wa tatu mfululizo kwa filamu za Tanzania kushinda tuzo ya filamu bora kwenye tamasha hilo, ambapo jumla ya filamu 2,810 kutoka mataifa 32 duniani zilikuwa katika kinyanga’anyiro hicho.

 

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button