FILAMU 11 zilizoshinda katika tamasha la filamu la nchi za majahazi ( ZIFF), zinatarajiwa kuoneshwa Tanzania Bara kuanzia Novemba 27 mwaka huu.
Mkurugenzi wa ZIFF, Profesa Martin Muhando, akizungumza leo katika Kituo cha Utamaduni Ufaransa jijini Dar es Salaam, amesema katika filamu hizo 11, filamu nne ni za Tanzania ikiwemo Vuta Nikuvute ambayo imeteuliwa kuingia katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo za Oscar mwakani.
Ametaja filamu nyingine za Tanzania zitakazooneshwa ni Chumba Namba 61, Mvamizi na Kazija, wakati filamu saba zilizosalia zinatoka mataifa mbali mbali ikiwemo nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU)
Naye Balozi wa Hispania nchini, Jorge Moragas akizungumza kwa niaba ya nchi za EU, amesema umoja huo kwa kushirikiana na ZIFF wataonesha filamu hizo katika vyuo vikuu vya Tanzania Bara, lengo likiwa ni kuwajengea uelewa watengeneza filamu wa Tanzania Bara.
Vyuo vitakavyoonyeshwa filamu hizo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Bagamoyo na Iringa.
“Watayarishaji wa filamu wa Tanzania Bara watapata fursa ya kuona kazi mbalimbali za wenzao na kujifunza,”amesema