Firmino kusepa Liverpool
Mshambuliaji wa Liverpool. Roberto Firmino ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu, kwa mujibu wa ripoti.
Timu hiyo inataka kumuandalia sherehe ya mkono wa kwaheri. Mbrazil huyo alitua Liverpool Juni 24, 2015 kwa dau la Pauni milioni 29 kutoka Hoffenheim ya Ujerumani.
Mpaka sasa nyota huyo amecheza michezo 353, amefunga mabao 107 na kutoa pasi za mabao 71.
Katika michezo hiyo, Firmino ameshinda mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu England, FA Cup, League Cup, Club World Cup na Uefa Super Cup.