Fisi aua mtoto akitafuta kuni

MTOTO Eliud Jarome (2) ameuawa baada ya kushambuliwa na fisi akiwa na watoto wenzake wakitafuta kuni katika Kata ya Zugimlole Tarafa na Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.

Akizungumza na vyombo vya habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao alisema kwamba tukio hilo lilitokea Aprili 5, mwaka huu.

Alisema kwamba kwa kuwa mtoto huyo alikuwa mdogo hakuweza kukimbia na hivyo kushambuliwa na fisi.

Advertisement

Kamanda Abwao alisema kwamba  askari wa wanyamapori walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumuua fisi huyo.

Wakati huo huo polisi mkoani humo imewataka wananchi kuelekea kwenye ibada na sherehe za Sikukuu ya Pasaka washerehekee kwa amani na utulivu kwa kufuata sheria za nchi.

Kamanda Abwao aliwataka madereva wa vyombo vya moto wajiepushe na mwendo kasi, kupita magari mengine sehemu hatarishi na kutumia kilevi cha aina yoyote wakati wakiendesha vyombo vya moto.

Aliwataka pia wananchi kuendelea kushirikiana na polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu ili kuendelea kuuweka mkoa katika hali ya usalama.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *