TIMU ya wasichana ya Fountain Gate imeibuka mabingwa wa michuano ya Shule za Secondari inayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) baada ya kuifunga mabao 3-0 timu ya Ecole Omar IBN Khatab kutoka nchini Morocco kwa mabao 3- 0.
Ushindi huo unaifanya Fountain Gate kuvuna kitita Cha Dola 300,000 sawa na Sh milioni 697 kama Mabingwa wa mashindano hayo Afrika katika Fainali hizo zilizoshuhudiwa pia na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma.
Kabla ya mchezo huo wa fainali Faountain Gate ilicheza mechi ya nusu fainali dhidi ya timu ya wasichana ya Csg De Mfilou kutoka DR Congo na kuiibuka na ushindi wa mabao 4-0, huku mshambuliaji Winfrida Hubert akifunga mabao matatu peke yake na hiyo kuwa hat-trick yake ya pili kwenye mashindano hayo.
Miongoni mwao ni Rais wa Caf, Patrice Motsepe, Mawaziri wa Michezo kutoka nchi washiriki wa mashindano hayo na Tanzania ikiwakilishwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma na Rais wa TFF, Wallace Karia