Fountaine Gates chachu soka la wanawake, wanaume

SOKA la wanawake ni mchezo unaokuwa kwa kasi zaidi Tanzania, ni utamaduni wa wanawake kucheza mpira wa miguu umeanza kueleweka kwa wengine, ingawa bado kuna kundi kubwa halijaelewa.

Katika kukuza soka la wanawake, serikali imekuwa ikiandaa programu mbalimbali za kukuza na kuendeleza mchezo huo ikiwemo Michezo kwa Shule za Msingi Tanzania (Umitashumta) na Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (Umiseta). Pamoja na mpango huo wa serikali pia taasisi zisizo za kiserikali zimeanzisha shule maalumu za sekondari ya kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo kwa watoto wa kike na wa kiume.

Shule ya Fountain Gate wenye makao yake makuu mkoani Dodoma ni kati ya taasisi binafsi inavyoendesha shule maalumu zinazoibua vipaji na kuviendeleza ukiwemo mchezo wa mpira wa miguu kwa wasichana. Kutokana na vipaji vilivyoibuliwa na kuendelezwa hasa katika soka la wanawake, timu ya Fountain Gate imeweza kushiriki mashindano makubwa ya soka la wanawake kwa shule Afrika.

Katika ushiriki huo mwaka huu imetwaa ubingwa wa Mashindano ya Shule ya Afrika yaliyomalizika hivi MAKALA FOUNTAIN GATE karibuni jijini Durban, Afrika Kusini baada ya kuifunga timu ya Morocco ya Ecole Omar IBN Khatab kwa mabao 3-0 katika mchezo wa fainali.

Nyota wa mashindano hayo na mfungaji bora ni wa kutoka timu ya Fountain Gate, Winfrida Gerald (19), ambaye ni mzaliwa wa Ifakara, Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro. Winfrida amezaliwa mwaka 2004 akiwa mtoto wa tatu kati ya wanne wa familia ya mzee Gerald, ambao wawili ni wanaume na wawili wa kike.

Mfungaji bora wa mashindano hayo anasema kuwa hakuamini kile kilichotokea katika mashindano hayo makubwa Afrika hadi kutwaa taji hilo. Anasema haikuwa rahisi kwake kuamini wao ni mabingwa, kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kushiriki mashindano makubwa na wakati huo hakuwa na muda mrefu tangu ameanza kucheza soka la wanawake shuleni hapo.

Nyota huyo katika mashindano hayo makubwa Afrika, ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule hiyo anasema ilitokea kuupenda mchezo wa mpira wa miguu tangu akiwa na umri mdogo. Kutokana na mafanikio mazuri yanayopatikana katika mchezo wa soka, anawashauri watoto wa kike wengine kujitokeza kwa wingi kuupenda na kucheza soka la wanawake.

Winfrida anawasihi wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao shuleni na kwamba wasiwakatalie pindi wanapopenda kucheza michezo ya aina mbalimbali kwa sababu michezo hivi sasa ni ajira, michezo inajenga afya, utimamu wa mwili na masomo shuleni.

Anasema kwake yeye siri na mafanikio anayoyapata ni kutokana na kujituma, kupambana, kuwasikiliza walimu, kujituma na kushirikiana vizuri na wachezaji wenzake. “Siri ya mafanikio yangu ni kuzingatia mambo hayo na hasa ukizingatia kuwa mimi sijaanza kucheza zamani ni juzi juzi tuu kwenye nafasi hii ya mshambuliaji,” anasema Winfrida.

Winfrida anasema wakati wote wa mashindano hayo wachezaji hawakuogopa maumbo makubwa ya wachezaji wa timu pinzani na hilo liliwasaidia kuwa na ujasiri wa ushindi kwenye kila mchezo. Winfrida anasema ndoto yake ni kufika mbali katika mchezo huo na kwamba anapambana ili aweze kutimiza malengo yake ya baadaye kuwa mchezaji mkubwa wa kimataifa Katika kuendeleza michezo nchini ameiomba serikali na viongozi wa ngazi mbalimbali waendelee kuimarisha sekta za michezo ili watoto wengi waweze kujitokeza kukuza vipaji vyao kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

Kabla ya mchezo wa fainali, Fountain Gate ilicheza mechi ya nusu fainali dhidi ya timu ya wasichana ya Cag De Mfilou kutoka DR Congo na kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 huku mshambuliaji, Winfrida akifunga mabao matatu peke yake na hiyo kuwa ‘hat-trick’ yake ya pili.

UONGOZI WANENA Naye Mkuu wa wakuu wa shule za Fountain Gate, Joseph Mjingo anasema kufanikiwa kuwa mabingwa kwa ngazi ya Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kumewawezesha kupata Dola za Marekani 100,000 (sawa na Sh 235,314,000). Baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika, Fountain Gate wamepata Dola za Marekani 300,000 (ambazo ni sawa na Sh milioni 707) na hivyo kuondoka na jumla ya Dola za Marekani 400,000.

Mjingo anasema fedha hizo wanatakiwa kuandika andiko la mradi wa miundombinu kupelekwa kwenye taasisi hizo ili fedha ziweze kutolewa na moja kwa moja kwenda katika miradi iliyokusudiwa. “Ndiyo maana tumepita Morogoro na kuyazungumza haya na tayari tumeshakuwa

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x