Freddie Roman afariki dunia

TAARIFA za kusikitisha kutoka nchini Marekani mkali wa kuvunja mbavu, Freddie Roman amefariki. Taarifa ya binti yake Judi Levin imeeleza.

Roman alikuwa muigizaji/mwandishi/mtayarishaji wa maudhui mbalimbali amefariki jana jioni katika hospitali moja huko Boynton Beach, Florida, hii baada ya kupata mshtuko wa moyo asubuhi nyumbani kwake. Judi Levin ameeleza.

Mchekeshaji huyo alitumbuiza katika kumbi nyingi zenye hadhi ikiwemo Caesars Palace huko Vegas na Harrah huko Atlantic City.

Roman aliigiza katika filamu nyingi zikiwemo: Karibu kwenye Kutsher’s: The Last Catskills Resort (2012), The Last Laugh (2006), Bittersweet Place (2005), Christ in the City (2005) na nyingine nyingi.

Pia alionekana kwenye vipindi vingi vya TV vikiwemo: Law & Order: Criminal Intent, Now That’s Funny!, Stark Raving Mad, The Tonight Show Starring Johnny Carson kutaja chache.

Habari Zifananazo

Back to top button