‘Fungafunga’ amejipata?

DODOMA: Mwamba Freddy Kouablan ni kama amejitafuta na sasa anaelekea kujipata, licha ya kutokubalika na baadhi ya Mashabiki wa @simbasctanzania tayari ameweka mabao Sita nyavuni kwenye Ligi Kuu msimu huu licha ya kusajiliwa kipindi cha dirisha dogo la usajili.

Isome pia: https://habarileo.co.tz/simba-yafufukia-unguja/

Kwa washambuliaji asilia yaani namba 9 wanaocheza kwasasa kwenye Ligi Kuu, Freddy amezidiwa mabao na Waziri Junior wa KMC mwenye mabao 12, Samson Mbagula wa Tanzania Prisons mwenye mabao 08 na Adam Adam wa Mashujaa mwenye mabao 07.

Isome pia: https://www.instagram.com/p/C7GtVevoIo9/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

Wengine waliomzidi ni viungo kutoka timu mbalimbali wanaocheza Ligi kuu kwa sasa.

Hata hivyo Freddy amebakiza mabao 02 kumfikia mtangulizi wake Jean Baleke aliyefunga mabao 08 kabla ya kutimkia nchini Libya.

Je ‘Fungafunga’apewe muda msimu ujao atajipata zaidi?

Habari Zifananazo

Back to top button