‘Fursa kibao sekta ya madini’

DODOMA: SEKTA ya madini itachangia pato la taifa kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.

Hatua hiyo inataokana na mikakati mbalimbali ikiwemo kufanya mabadiliko ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010, yaliyotekelezwa mwaka 2017, hivyo kuundwa Tume ya Madini.

Mikakati hiyo imebainishwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

“Kuanzia mwezi Julai hadi Septemba, 2023 Tume ya Madini imepokea maombi mapya ya leseni za madini 7596. Yote yaliidhinishwa baada ya kukidhi vigezo,” amesema mhandisi huyo.

Amesema katika ukusanyaji maduhuli kuanzia Julai hadi Septemba 2023, Tume ya Madini imekusanya Sh bilioni 184.53.

“Mikakati kabambe imewekwa na tume kuhakikisha lengo la kukusanya Sh bilioni 882.12 linafikiwa katika mwaka wa fedha 2023-24,” amesema Samamba.

Amesema tume inahimiza wananchi kuwekeza katika sekta ya madini, kuanzia kwenye uchimbaji, uchenjuaji, biashara na utoaji huduma migodini.

“Bado tunaendelea na uhamasishaji wa wachimbaji wadogo wa madini wasio rasmi kuwafanya rasmi kwa kuwasajili sambamba na kutatua changamoto ili uchimbaji wao ulete tija,” ametanabahisha kiongozi huyo.

Amewataka wadau wa madini nchini kufanya shughuli zao kwa uzalendo, kufuata sheria ya madini na kanuni zake sambamba na kujiepusha na vitendo vya utoroshaji wa madini.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
MONENY
MONENY
1 month ago

CCM bila siasa za KUJENGA BARABARA, HOSPITALI, KUMSIFIA RAIS, SHULE, NYUMBA ZA WATUMISHI WA UMMA MTAKUWA NA SIASA GANI!?

KUMBE KUJENGA MILELE

Capture.JPG
Whitney Holland
Whitney Holland
Reply to  MONENY
1 month ago

Making extra salary every month from house more than $15,000 just by doing simple copy and paste like online job. I have received $18,000 from this easy home job. Everybody can now makes extra cash online easily.

By Just Follow………….. http://Www.Smartwork1.Com

MONENY
MONENY
1 month ago

CCM bila siasa za KUJENGA BARABARA, HOSPITALI, KUMSIFIA RAIS, SHULE, NYUMBA ZA WATUMISHI WA UMMA MTAKUWA NA SIASA GANI!?

KUMBE KUJENGA MILELE…

Capture.JPG
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x