Fursa kimaisha zimeongezeka – Paulina Onna

DAR ES SALAAM: MKE wa msanii Dogo Janja anayejulikana kwa jina la Paulina Onna maarufu ‘Quenlinnatotoo’amesema amesema baada ya kupata mtoto wa kiume ‘Ahyan’ fursa za kimaisha zimeongezeka mara dufu.

Akizungumza na HabariLEO, Queenlimtoto’ ambaye ni meneja wa kampuni Geniusjini_66 amesema majukumu ya malezi hayamnyimi kufanyia kazi fursa anazozipata kwasababu mtoto pia amekuwa kwa kiasi.

“Ukiwa mama hata roho inabadilika unakuwa mtu mwingine kabisaa kila kitu chako kinabadilika hata mtindo wa maisha pia unabadilika sababu unapoishi unaishi pia kwa ajili ya hicho kiumbe kizuri ulichokileta hapa duniani,” ameiambia HabariLEO.

Queenlimtoto amesema haoni changamoto yoyote kwenye suala la malezi anafurahia kulea kwanj kabla ya mtoto huyo tayari alishakuwa nao.

“Kabla ya kuwa na mtoto tayari nina watoto ambao nawatambua kama watoto wangu kwa hiyo hapo kwenye idadi ya watoto sina hesabu nazoweza kukupa napenda watoto nalea watoto wengi zaidi,”

Amesema baada ya mtoto wake kukua hatoweza kumchagulia kazi yake au baba yake ‘Dogo Janja’ bali atachopenda mtoto huyo basi atamuachia afanye.

Habari Zifananazo

Back to top button