G Nako amtabiria ushindi bondia Nassib Ramadhan
DAR ES SALAAM; Msanii wa hip hop George Sixtus ‘G Nako’ amesema bondia Nassibu Ramadhani, atamkalisha Juma Choki kwenye pambano liitwalo Dar Boxing Derby Juni 29, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, G Nako amesema ana imani kubwa na Nassibu Ramadhani kutokana na maandalizi anayoendelea kufanya, huku akimtahadharisha mpinzani wake.
“Nina imani kubwa na Ramadhan amejipanga, atapigwa huyo Juma Choki kwa KO,” amesema msanii huyo.
Mapambano mengine siku hiyo ambayo yatafanyika viwanja vya Posta Kijitonyama, Dar es Salaam ni Haidary Mchanjo dhidi ya Charles Tondo, Loren Japhet na Issa Peche, Bonny Sela na Adam Ngange, huku Oscar Richard akivaana na Tonny Rashid