Gamondi atangaza Kiama kwa Asas Djibouti kesho

DAR ES SALAAM: Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema bado hawajamaliza kazi kuelekea mchezo wa mkondo wa pili siku ya kesho dhidi ya Asas Djibouti katika hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.

Kocha huyo ameyasema hayo leo Agosti 25, 2023 wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.

Muargentina huyo amesema licha ya kutengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo wa kwanza walishindwa kuzitumia hivyo anaamini kesho utakuwa ni mchezo wa tofauti na wataingia na mbinu mpya ili kupata ushindi na kusonga mbele.

Advertisement

Yanga wataingia kwenye mchezo huo utakaopigwa kesho kwenye dimba la Azam Complex Chamazi wakiwa na uongozi wa bao 2-0 waliopata juma lililopita.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *