Gamondi baba lao Ligi Kuu

DAR ES SALAAM: KOCHA wa Young Africans SC, Miguel Gamondi ametwaa tuzo ya Kocha Bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Gamondi ameiongoza Young Africans katika michezo mitano mwezi huu kwa kushinda michezo minne na kutoka sare mchezo mmoja na kuiwezesha klabu hiyo kutoka nafasi ya pili hadi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi.

Young Africans ilitoka 0-0 na Kagera Sugar, ikazifunga Dodoma Jiji bao 1-0, Mashujaa 2-1, Prisons 1-2 na KMC 0-3.

Gamondi amewashinda Abdelhak Benchikha wa klabu ya Simba na Ahmad Ally wa Tanzania Prisons alioingia nao katika kinyang’anyiro hicho.

Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Azam Complex, Amir Juma kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Februari.

Habari Zifananazo

Back to top button