KUELEKEA mchezo wa kesho Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga imefanyia kazi maeneo mawili ya uwanja, eneo la kushambulia na kujilinda, kocha Miguel Gamondi ameeleza akifafanua umuhimu wa maeneo hayo.
Akizungumza na wanahabari leo Februari 23, 2024, Gamondi amekiri kuwa mchezo huo utakuwa mgumu, hivyo wanapaswa kufahamu ni wakati upi wa kutekeleza majukumu yapi.
“Mchezo utakuwa mgumu na utakuwa ni mchezo wenye mbinu nyingi hasa wakati gani wa kushambulia na wakati gani wa kujilinda”. Gamondi ameeleza.
Gamondi amesema wachezaji wake wanapaswa kutumia kila nafasi watakayoipata, kisha ulinzi kwenye eneo la mwisho utafuata.
“Tutahakikisha tunatumia vizuri kila nafasi tutakayoipata kwenye mchezo wa kesho”. Gamondi amesema.