Gamondi: Mbona freshi tu

KOCHA Mkuu wa klabu ya Yanga Miguel Gamondi amesema hana shinikizo lolote kuelekea msimu ujao na anaimani yakufanya vizuri akiwa na timu hiyo.

Miguel amezungumza na Habari leo/ Spotileo Julai 19, 2023 na kusema yupo tayari kuianza safari yake huko Jangwani.

Kocha huyo raia wa Argentina amesema kwa muda mchache aliokaa na kikosi chake amewaona wachezaji wanaojituma na kujitambua kitu ambacho kinampa imani ya kufanya vizuri na timu hiyo na hana wasiwasi wowote.

” Nimezoea kufanya kazi katika shinikizo hasa katika soka la Afrika, mashabiki wanahitaji matokeo muda wote kwa hiyo ni lazima ukiwa kocha ujue kuishi katika nyakati zote ukiwa umeshinda au umepoteza”amesema Gamondi

Alipoulizwa kuhusu kivuli cha benchi la ufundi lililopita ndani ya timu hiyo kocha Miguel amesema anaheshimu kile kilichofanywa na watangulizi wake na anatamani kufanya zaidi ya walipoishia ndio maana ameanza mapema kukisuka kokosi hicho.

Kocha huyo ameongeza kwa kusema kuwa anavutiwa mno na mazingira ya Tanzania hasa tamaduni za mashabiki wa soka la bongo kujitokeza kwenye matukio mbalimbali yanayoihusu timu zao.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button