Gamondi: Rekodi ya kuvunja dhidi ya Simba? hakuna
DAR ES SALAAM: KOCHA wa Yanga Miguel Gamondi amesema hana rekodi yoyote ya kuvunja dhidi ya Simba kwani hajawahi kupoteza dhidi ya timu hiyo.
Kocha huyo amesema katika mchezo mmoja aliocheza dhidi ya Simba alipata sare lakini wapinzani wake walifaidika kwa changamoto ya mikwaju ya penati kitu ambacho yeye anaaminini alimaliza kazi yake ndani ya dakika 90.
Ameongeza kuwa kinachokwenda kutafutwa uwanjani kesho ni heshima ya Klabu ya Yanga na sio ya kocha wa Yanga.
Kocha huyo raia wa Argentina amesema anaamini wachezaji wa Yanga na Simba wana uwezo mkubwa na watatoa burudani ya aina yake kwenye mchezo wa kesho katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.
” Ninaamini taifa lifafurahi kuhusiana na mchezo huu unazozikutanisha timu kubwa mbili katika soka la Tanzania utakuwa wa tofauti sana na mchezo uliopita kwa sababa vitu vingi ni vya tofauti kwanza uwanja ni mwingine, lakini pia hili ni shindano jingine” amesema.