Gamondi: ‘Rotation’ niacheni mimi na timu yangu

DAR ES SALAAM: Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema  watu wengi wanahoji kwanini hatoi nafasi ya wachezaji wengine kupata nafasi kwenye kikosi chake ‘Rotation’ lakini yeye anajua kwanini anafanya hivyo.

Gamondi amesema watu wanaohoji jambo hilo ndio walewale waliozungumza siku alipofanya mabadiliko kwenye mchezo dhidi ya Ihefu mchezo ambao Yanga walitandikwa mabao 2-1 mkoani Mbeya.

Nakumbuka mchezo dhidi ya Ihefu nilifanya ‘Rotation’ nikawapanga akina Diarra, Bakari, Kibwana Moloko, Skudu, Mzize na niwaambie tuu hawa ni wachezaji wakubwa sikupanga timu ya vijana lakini tulifungwa, hatukufungwa kwasababu ya ‘Rotation’ tulifungwa kwasababu hata msimu uliopita tulifungwa pia.

Kocha huyo ameongeza kuwa haoni sababu ya kufanya mabadiliko ikiwa bado anaendelea kupata ushindi katika michezo ambayo anacheza na atafanya mabadiliko ikiwa yeye na benchi lake la ufundi wataona ipo haja ya kufanya hivyo.

Kesho Yanga watashuka dimbani kuwavaa Mtibwa Sugar kwenye muendelezo wa Ligi kuu Tanzania Bara.

 

Habari Zifananazo

10 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button