Gamondi: Waacheni waje makundi!

DSM: DROO ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika tayari imeshajulikana kuanzia saa 10 alasiri leo na sasa timu zinaanza kusomana, ili ifikapo Novemba 24 michezo ya kwanza itakapoanza zimudu kufanya vyema.
Yanga amepangwa Kundi D pamoja na mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri, CR Belouizdad ya Algeria na Medeama ya Ghana.
Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema timu yake ipo tayari kukutana na mpinzani yoyote katika michuano ya Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi.
Gamondi amesema hatua hiyo ya makundi haina uchaguzi wa kupangwa na nani muhimu ni kupambana na kusonga mbele.
“Bahati nzuri timu ipo vizuri na ilishajua mapema imefuzu makundi na itakuwa tayari kupambana na kusonga mbele zaidi, kwani mashabiki wana kiu ya kuona kile kilichotokea Kombe la Shirikisho msimu uliopita kinajirudia tena Ligi ya Mabingwa, ”amesema.
Kwa upande wa Meneja wa timu hiyo Walter Harrison amesema kuwa makundi wameyaona na amekiri ni kundi gumu.
Mechi za kwanza hatua ya makundi zitachezwa rasmi kati ya Novemba 24 hadi 26 mwaka huu.
2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *