KIUNGO wa Barcelona, Pablo Gavira ‘Gavi’ leo atafanya upasuaji baada ya kuumia goti wiki moja iliyopita katika mchezo wa kufuzu Euro2024 kati ya Hispania na Georgia.
Pablo kwa mara nyingine ameongozana na wakala wake Iván de la Peña katika zoezi hilo.
Baada ya upasuaji huo, Gavi atarejea uwanjani tena msimu ujao hata hivyo atakosa michuano ya Euro.