Gavi kukosa Euro 2024
*BREAKING*: KIUNGO wa Barcelona na Hispania, Pablo Gavi atakosa michuano ya Euro2024 kutokana na jeraha la goti.
–
Gavi aliumia katika mchezo wa Hispania dhidi ya Georgia ulioisha kwa timu yake kushinda mabao 3-1 jana.
–
Taarifa za madaktari wa Barcelona zinaeleza kiungo huyo atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 8-9.
–
Gavi atarejea kwenye maandalizi ya msimu mpya wa 2024-2025.