Gavu: Wekezeni elimu ya dini kwa watoto
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Idara ya Organaizesheni Issa Gavu amesema kuwa kuwekeza katika elimu ya Dini kwa vijana nikuwajengea nyezo muhimu ya kimaadili isiyofutika katika maisha yao.
Aidha, amesema kuwa wakati wazazi wakiendelea kuwekeza elimu ya jumla kwa watoto, wasisiahau kuwekeza pia kwenye elimu ya dini kwani ndio inayowajenga zaidi vijana kiimani na imani hudumu zaidi kwa katika nyoyo za watu.
Gavu ameyasema hayo wakati aliposhiriki Mashidano ya Qur’an leo April 9, 2023 katika Jimbo la Mafia mkoani Pwani.
Tukio hilo liliondaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo na Naibu wa Waziri wa Elimu, Sanyasi na Teknolojia Mhe. Omari Juma Kipanga.