Geita yaachana na Mpole

UONGOZI wa klabu ya Geita Gold umethibitisha kuachana na mshambuliaji George Mpole kwa sababu ambazo hawajaziweka wazi.

Katika taarifa yao kwenda kwa mchezaji huyo, Geita imesema kuanzia sasa mchezaji huyo yupo huru kwenda katika klabu anayohitaji kufuatiwa makubaliano ya pande zote kati yake na klabu.

Geita imemtakiwa kila la heri mchezaji huyo katika majukumu yake mengine. Mpole aliwahi kuhusishwa na klabu kadhaa kipindi cha nyuma, ikiwemo Azam FC, yenye maskani yake Chamanzi Dar es Salaam.

Mpole alitwaa kiatu cha mfungaji bora wa ligi kuu TZ Bara msimu wa 2021/22 kwa kufunga magoli 17 ndani ya klabu hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button