Gen Z waingia tena mitaani Kenya

MAANDAMANO ya vijana wanaojulikana Gen Z yanaendelea nchi Kenya licha ya Rais William Ruto kupanga kukutana kwa njia ya mtandao na vijana hao Julai 4.

Vijana hao leo wameingia mitaani katika miji kadhaa ya Kenya ukiwemo mkuu mkuu, Nairobi wakitaka serikali kufanya mabadiliko mbalimbali.

Miji mingine ilikumbwa na maandamano hayo ni Kisumu, Kajiado, Nakuru na Kisii

Ingawa mahakama imepiga marufuku matumizi ya mabomu ya machozi na maji ya kuwasha dhidi ya waandamanaji lakini polisi wa kutuliza ghasia wamevyatua mabomu hayo katika baadhi ya maeneo.

Vyombo vya Habari vya Kenya vimeripoti kuwa maandamani yaliyoingia wiki ya tatu yamesababisha vifo vya watu 39 huku wengine Zaidi ya 300 wakijeruhiwa.

Habari Zifananazo

Back to top button